Benni McCarthy kuifunza klabu ya Ubelgiji

Image caption McCarthy

Mshambuliaji wa zamani wa taifa la Afrika Kusini Benni McCarthy ndio mkufunzi mpya wa klabu ya Ubelgiji Sint-Truidense.

Amesema kuwa anataka kumuigiza kocha wa Chelsea Jose Mourinho baada ya kucheza chini ya mkufunzi huyo alipokuwa akiichezea klabu ya Porto nchini Ureno.

''Alikuwa kocha mkakamavu na mwenye maono na akili ya kucheza mpira'',McCarthy aliambia BBC.