RIPOTI ZA MOJA KWA MOJA ZA MECHI ZA LIGI KUU YA UINGEREZA

Katika michuano ya leo,Crystal palace inakabiliana na West Brom Wich Albion nayo Aston Villa ikiialika Stoke City.Mancity nayo inamenyana na Newcastle.

19.00pm:Matokeo

Crystal Palace 2 - 0 West Brom

Aston Villa 0 - 1 Stoke

Bournemouth 1 - 1 Watford

Man City 6 - 1 Newcastle

Norwich 1 - 2 Leicester

Sunderland 2 - 2 West Ham

Image caption Kocha wa Newcastle

Na mechi inakamilika ikiwa Mancity 6-1 Newcastle.

Image caption Aguero

18.24pm: Mancity yafanya mabadiliko hapa Aguero atoka baada ya kuifungia timu yake mabao 5 pekee

18.21pm:Aguerooooooooo Gooooooooal .Amini usiamini Aguero aifungia City bao la 5 na la sita kwa Mancity dhidi ya Newcastle

18.13pm:Goooooal De Bryne wa Manchester City aifungia City bao lake la nne hapa do.mambo yamegeuka na kuwa mabaya kwa Newcastle.Hiyo inamaanisha kwamba ile rekodi ya kocha McClaren ya kutofungwa na Mancity imevunjwa.

Image caption Aguero aubusu mpira baada ya kufunga mabao matatu

18.09pm:Goooooooal Aguero aifungia Manchester City bao la tatu na kuzima kdomo cha Newcastle.Je Newcastle itaweza kuhimili mchezo wa City?yetu ni macho

18:05Pm:Gooooooooal Aguero afunga bao la pili.

17.52pm:Na kipindi cha kwanza cha mechi kinakamilika

Image caption Aguero

17.42pm:Gooooooooal baada ya kukosa mabao ya wazi hatimaye Kun Aguero anasawazisha hapa na kufanya mambo kuwa City 1-1 Newcastle

Image caption Wachezaji wakabiliana

17.34pm:Agueroooooo, nje akosa bao la wazi hapa mshambulijia huyu matata

17.30pm: Raheem Sterling anajaribu kupenya katika lango la Newcastle lakini safu ya ulinzi ya Newcastle iko imara

Image caption Raheem Sterling

17.27pm:Manchester city sasa yaamka na kusema wacha tuwachezee ngoma.dakika ya 28 City 0 Newcastle 1

17.27pm:Mchezaji Mitrovic akosa bao jingine la wazi hapa ambapo angefanya mambo kuwa mawili.do

17.23pm:Manchester City wajaribu kutafuta bao la kusawazisha kupitia Aguero lakini mabeki wa Newcastle wakataa

Image caption Mitrovic

17.17pm:Goooooooooal Newcastle wapata bao lao la kwanza kupitia Aleksander Mitrovic

17.11pm:Aguero afanya shambulizi la kichwa lakini mabeki wa Newcastle waokoa.

17.09pm:Mancity yaanza kwa kulivamia lango la Newcastle huku wageni hao wakionekana kujaribu kulilinda lango la kwa sasa

17.00pm:Mechi kati ya Mancity na Newcastle yaanza

Image caption McClaren

16.56pm:Kocha wa Newcastle McClaren hajawahi kupoteza dhidi ya klabu ya Manchester City,je mkoko utaalika maua leo?

Image caption Mancity
Image caption Newcastle

MECHI KATI YA MANCHESTER CITY vs NEWCASTLE

16.36pm:Na mechi kati ya Crystal palace dhidi ya West Brom Wich inakamilika ikiwa Crystal palace 2-0 West Bromwich

16.27pm:Arsenal v Man Utd:

Haki miliki ya picha epa
Image caption Theo Walcot

Je. unadhani Theo Walcot ndio mchezaji anayetarajiwa kuwa tegemeo la mashambulizi Arsenal?.

Tangu aliyekuwa mashambuliaji wa Arsenal Thierry Henry aseme kwamba Arsenal haitashinda ligi ya Uingereza hadi pale safu ya ushambulizi itakaporekebishwa, harakati za kumtafuta mshambuliaji huyo zimekuwa zikigonga vichwa vya habari.Je unadhani Theo Walcot ndiye Jibu la tatizo hilo?

16.31pm:Gooooooooal Yohan Cabaye aipatia crystal palace bao la pili baada ya kufunga penalti.Crystal palace 2-0West Brom Wich

Image caption bollasie

16.10pm:Gooooooooooal Bollasie aiweka kifua mbele crystal palace baada ya kupata krosi nzuri aliyoipiga kichwa na kumwacha mlinda lango wa West Brom bila jibu.

Crystal Palace 1-0 West Brom daika ya 57

Image caption Crystal palace

16.01pm:Wachezaji wa Stoke wanaonekana kulemewa na sasa wameamua kurudi nyuma ili kulinda lango la.

15.59pm:Jason Puncheon na Yannick Bollasie waanaonekana kuongeza nguvu katika safu ya mashambulizi ya Crystal Palace lakini bado bahati haijasimama.

15.56pm:Zaha anaonekana kuonyesha umahiri wake wakati anapokuwa na mpira ,anaweza kwenda pande zote kwa kasi lakini mara nyingine anachanganyikiwa anapokuwa na mpira.

15.53pm:Mabadiliko, West Bromwich Albion. Craig Gardner achukua mahala pale Saido Berahino.

Image caption Wlfried Zaha

15.50pm:Kipindi cha pili cha mechi kati ya crystal palace na West Bromwich chaanza

15.33pm:Na kipindi cha kwanza cha mechi kati ya Crystal Palace dhidi ya West Brom kinakamilika

15.27pm:Crystal palace yaendelea kutawala mechi huku washambuliaji wake wakizidi kulishambulia lango la West Bromwich

Wachezani Wilfried Zaha na Jason Puncheon pamoja na Yannick Bollasie wamefanya mashambulizi chungu nzima.

Image caption West Ham kumenyana na Sunderland

15.20pm:Mechi kati ya Sunderland dhidi ya West kuchezwa mwendo wa saa kumi na moja saa za Afrika mashariki.

15.00pm:Crystal Palace inatafuta bao kwa udi na uvumba kupitia Zaha ambaye liocha ya kuwahangaisha mabeki wa WEst Brom bahati yake haijasimama

2.30pm.Mechi kati ya Crystal Palace na West Brom Wich Albion

Image caption Saido Berahino wa West Bromwich Albion

Orodha ya watakaocheza

Crystal Palace

13 Hennessey34 Kelly06 Dann04 Hangeland23 Souaré18 McArthur07 Cabaye11 Zaha42 Puncheon10 Bolasie16 Gayle

Substitutes

03 Mariappa08 Bamford09 Campbell12 McCarthy26 Sako28 Ledley41 Gray

Image caption West brom ndio timu ya pekee katika ligi ya Uingereza ambayo haijafungwa bao ugenini msimu huu

West Bromwich Albion

13 Myhill25 Dawson23 McAuley06 Evans11 Brunt24 Fletcher05 Yacob07 Morrison14 McClean Booked33 Rondón18 Berahino

Substitutes

04 Chester08 Gardner10 Anichebe16 Gamboa17 Lambert19 McManaman21 Lindegaard

2:00pm.Orodha ya mechi za ligi kuu ya Uingereza siku ya jumamosi

Crystal Palace 0 - 0 West Brom 2.45pm

Aston Villa v Stoke 5:00pm

Bournemouth v Watford 5:00pm

Man City v Newcastle 5:00pm

Norwich v Leicester 5:00pm

Sunderland v West Ham 5:00pm

Chelsea v Southampton7:30pm