Brendan Rodgers afukuzwa Liverpool

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Brendan Rodgers,afutwa kazi

Klabu ya soka ya Liverpool ya nchini Uingereza imemfukuza Meneja wake Brendan Rodgers baada ya matokeo mabaya ya muda mrefu.

Uamuzi wa kumfuta kazi Rodgers ulifanywa hata kabla ya mchezo ulioisha kwa suluhu dhidi ya Everton ambao uliwaacha Liverpool katika nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi ya England.

''Licha ya kuwa huu umekuwa ni uamuzi mgumu,tunaamini itatupa nguvu zaidi uwanjani,''ilisema taarifa ya klabu.

Meneja wa zamani wa klabu ya Chelsea na Real Madrid Carlo Ancelotti,kocha wa Ajax Frank de Boer na meneja wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund wamehusishwa kujiunga na klabu ya Liverpool katika siku za karibuni baada ya timu hiyo kuuanza msimu kwa kusua sua.