Kamati yataka Blatter asimamishwe kazi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sepp Blatter

Kamati ya maadili katika shirikisho la soka duniani FIFA imependekeza Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA asimamishwe kazi kwa siku tisaini.

Wanachama wa kamati hiyo walikutana wiki hii baada ya Jaji mkuu nchini Uswizi kufungua mashtaka ya uhalifu dhidi ya Blatter mwezi uliopita.

Blatter anatuhumiwa kwa kutia saini kandarasi zisizo na manufaa yoyote kwa FIFA mbali na kufanya 'malipo' kwa rais wa shirikisho la UEFA Michel Platini.

Blatter ambaye ni raia wa Uswizi amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka 1998 na Platini ambaye anataka kumrithi amekana madai yoyote ya kufanya uovu.

Hakuna uamuzi ulioafikiwa kuhusu kumchukulia hatua yoyote Platini.