Mkenya kupewa kandarasi mpya Southampton

Haki miliki ya picha v
Image caption Wanyama

Mkenya anayechezea soka ya kulipwa katika kilabu ya Southampton nchini Uingereza Victor Mugubi Wanyama ametupilia mbali harakati za uhamisho wake ambao haukufanikiwa alipotaka kuelekea kilabu ya Tottenham na sasa anasisitiza kuwa anaijali timu ya Southampton pekee.

Wanyama anayechezea safu ya kati alitaka kuhamia Tottenham ili kujiunga tena na mshauri wake Mauricio Pochettino katika kilabu ya Spurs kwa kufanya mgomo mnamo mwezi Agosti.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanyama

Lakini mkufunzi wa kilabu hiyo Ronald Koeman alisisitiza kuwa nyota wake si wa kuuza ili kuhakikisha kuwa anasalia St. Marys baada ya Wanyama kukataa kucheza dhidi ya Norwich.

Wakuu wa Southampton wana matumaini ya kumpatia kandarasi mpya mchezaji huyo kwa miaka mingine mitano.

Image caption Wanyama

Wanyama ameonekana akicheza vyema na kuiwezesha Southampton kupanda katika jedwali la ligi ya Uingereza.