Vumbi bado latimka mashindano ya Raga

Haki miliki ya picha
Image caption Mchezaji wa Raga

Mashindano ya Raga ya kombe la dunia yanayoendelea nchini England na Wales.

Leo kuna mechi mbili lakini ni bingwa mara mbili Afrika Kusini ambao wana nafasi nzuri zaidi ya kufuzu kwa robo-fainali.

Afrika Kusini inapambana na Marekani ikiongoza kundi B na pointi 11, na Scotland ni ya pili, huku Namibia ikipimana nguvu na Georgia.

Mataifa ambayo tayari yamefuzu kwa robo-faibali ni New Zealand, Argentina, Australia, Wales, Ireland na Ufaransa.

New Zealand ndio bingwa mtetezi baada ya kushinda Ufaransa pointi 8-7 katika kombe la dunia mwaka wa 2011.