Liverpool yateua meneja mpya

Image caption Jurgen Klopp

Liverpool imemteua Jurgen Klopp kuwa meneja wake mpya kwa mkataba wa miaka mitatu.

Klopp raia wa Ujerumani mwenye miaka 48 anachukua nafasi ya Brendan Rodgers aliyetimuliwa hivi karibuni baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa miaka mitatu na nusu.

Klopp amekuwa nje ya dimba tokea mwezi Mei mwaka huu baada ya kudumu na klabu ya Borussia Dortmund kwa misimu saba.

Anatarajiwa kuanza kazi kwenye klabu hiyo ya Liverpool na wasaidizi wake Zeljko Buvac na Peter Krawietz aliofanya nao kazi akiwa kwenye Ligi ya Bundesliga.

Klopp anatarajiwa kutambulishwa rasmi na klabu yake mpya siku ya Ijumaa katika mkutano na waandishi wa habari.

Alijiunga Dortmund mwaka 2008 na kuiongoza kushinda vikombe viwili vya ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga).