Michuano ya kimataifa, mbio za Baiskeli

Image caption Michuano ya mbio za baiskeli

Timu ya taifa ya Rwanda ya mchezo wa baiskeli inajiandaa kushiriki michuano ya nne ya kimataifa ya mbio za Biya nchini Cameroon.

Michezo hiyo itaanza Oktoba 14-18 mwaka huu.

Ushiriki wa Rwanda katika michuano hiyo ulithibitishwa siku ya jumatano na chama cha baiskeli nchini humo kupitia katibu mkuu wake Emmanuel Murenzi.

Timu hiyo ya Rwanda itakuwa ikijaribu kupata mafanikio mengine ndani ya mwezi mmoja baada ya kupata medali ya dhahabu kwenye mashindano ya All African games yaliyomalizikamwezi ulipita huko Kongo Brazaville.