Golikipa wa Newcastle kukaa benchi

Image caption Golikipa namba moja wa Newcastle, Tim Krul

Golikipa namba moja wa Klabu ya Newcastle Tim krul atakua nje ya uwanja kwa msimu mzima uliobaki.

Krul aliumia goti la mguu wa kulia wakati wa mchezo wa timu ya Taifa ya Uholanzi ikicheza na Kazakhstan kuwania kufuzu kucheza kombe la Ulaya

Golikipa huyo mwenye miaka 27 atarudi kwenye kambi ya timu yake Tyneside kwa matibatu zaidi, imesema taarifa ya klabu yake ya Newcastle.

Katika msimu huu wa ligi kuu ya England Krul amecheza michezo minane huku timu yake ikiburuza mkia

Kipa Freddie Woodman aliyekua kwa mkopo katika timu ya daraja la pili ya Crawley Town amerejeshwa katika timu hiyo.