Beki wa Liverpool nje msimu mzima

Image caption Beki wa kushoto wa Liverpool Joe Gomez atakosa mchezo wa Jumamosi

Beki wa kushoto wa klabu ya Liverpool, Joe Gomezatakua nje ya uwanja kwa msimu msimu uliobaki

Gomez mwenye umri wa miaka 18 aliumia goti akiichezea timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 mchezo dhidi ya Kazakhstan.

Kinda huyo amecheza michezo mitano ya ligi kuu msimu huu toka alipojiunga na Liverpool akitokea timu ya Charlton kwa dau la pauni million 3.5.

Kocha mpya wa Liverpool Jurgen Klopp anatarajia kuanza mchezo wake wa kwanza siku ya jumamosi dhidi ya Tottenham huku akikosa huduma ya beki huyo.