FA yamtoza faini Mourinho

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kocha wa Chelsea Jose Mourinho

Chama cha soka cha England FA, kimempa adhabu Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho kutokana na utovu wa nidhamu.

Mourinho amepewa adhabu ya kulipa Faini ya Pauni 50,000 pamoja na kufungiwa mchezo mmoja huku Kifungo hicho cha mchezo mmoja kinasimamishwa huku FA wakiangalia mwenendo wake.

Meneja huyo wa Chelsea alimshambulia kwa maneno mwamuzi Robert Madley aliyechezesha mchezo wao dhidi ya timu ya Southampton, na kuchapwa kwa mabao 3-1

Mourinho alikasirishwa na Refa Madley kutowapa Penati na kudai Waamuzi wanaogopa kutoa uamuzi kwa Timu yake.

Kauli hiyo iliwafanya FA wamfungulie Mashitaka ya Utovu wa Nidhamu wakidai kauli za Mourinho zinalenga kuonyesha Marefa wanapendelea.