Murray, Djokovic, Nadal wapeta Shanghai

Haki miliki ya picha AP
Image caption Andy Murray atamba Shanghai Masters

Muingereza Andy Murray anayeshika nafasi ya pili kwa ubora duniani kwa mchezo wa tenisi amemshinda Steve Johnson katika michuano ya Shanghai Masters

Murray ameshinda kwa seti 6-2 6-4, nyota huyu wa tenesi atachuana na John Isner wa Marekani katika hatua inayofuata.

Isner' alipata ushindi wa seti 6-3 7-6 (7-5)dhidi ya David Goffin wa Ubeligiji,

Nae mchezaji namba moja kwa ubora Novak Djokovic amesonga mbele katika raundi ya tatu kwa kumchapa Martin Klizan wa Slovakia kwa seti 6-2 6-1.

Rafael Nadal nae akapata ushindi katika mchezo uliotumia muda wa saa mbili na dakika 43, dhidi ya

Ivo Karlovic wa Croatia kwa seti 7-5 6-7 (4-7) 7-6 (7-4).