Ings nje ya dimba kwa msimu mzima

Image caption Mshambuliaji wa Liverpool, Danny Ings

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Dany Ings atakua nje ya uwanja kwa msimu mzima baada ya kuumia goti.

Ings mwenye miaka 23 aliumia goti wakati wa mazoezi ya klabu ikiwa ni siku moja tangu atoke kuitumikia timu ya taifa ya England kwa mara ya kwanza, kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za ulaya dhidi ya timu ya Lithuania.

Mshambuliaji huyu amefunga mabao matatu katika michezo saba aliyoichezea Liverpool akitokea Burnley.

Ings anakua mchezaji wa pili kuumia goti baada ya kinda Joe Gomez kuumia goti na kutakiwa kukaa nje ya uwanja kwa msimu mzima ili kutibu jeraha lake.