Lamar Odom apata fahamu siku 3 baadaye

Haki miliki ya picha AP
Image caption Odom akiichezea La Clippers

Mchezaji wa zamani wa mpira wa vikapu katika ligi ya NBA nchini Marekani Lamar Odom hatimaye amepata fahamu siku tatu baada kuzirai ndani ya danguro katika jimbo la Nevada.

Msemaji amesema kuwa bwana Odom alizungumza na kutoa maamkuzi ya kidole katika kitanda chake cha hospitalini.

Alikuwa katika mashine ya usaidizi baada ya kupatikana siku ya jumanne akitokwa na damu puani na mdomoni.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Odom na aliyekuwa mkewe Khloe Kardashian

Wafanyikazi wa danguro la Love Ranch,huko Crystal,Nevada wamesema kuwa bwana Odom alikuwa katika danguro hilo kwa siku kadhaa na amekuwa akila dawa za kulevya aina ya cocaine pamoja na zile za kuongeza hamu ya ngono.

Odom aliwahi kushinda taji la ubingwa akiichezea Los Angeles Lakers.