Australia yaifunga Scotland

Haki miliki ya picha
Image caption Mcheza Raga wa Australia akiwa na mwanae

Hatimaye Australia imefanikiwa kuifunga Scotland katika dakika moja ya mwisho ya mchezo katika mashindano ya kombe la dunia mchezo wa Raga hatua ya robo fainali.

Katika mchezo huo Scotland walikuwa wanaongoza lakini katika dakika ya mwisho Astaralia walipewa penati ambayo maamuzi yake yalikuwa ni ya mashaka . Wakati muda unaelekea kumalizika mwamuzi craig joubert akatoa uamuzi wa kuotea, lakini marudio yalionyesha kuwa adhabu hiyo haikustahili kutolewa kwani mpira ulimgusa mchezaji wa Austaralia.