Michel Platini asema bado anataka kumrithi Blatter

Haki miliki ya picha PA
Image caption Michael Platini

Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platini amesema bado ana moyo wa kutaka kumrithi Sepp Blatter kama Rais wa shirikisho la Kandanda duniani FIFA, licha ya kupigwa marufuku ya siku 90 ili kupisha uchunguzi wa madai ya ufisadi dhidi unaoendelea dhidi yake. Platini, mpaka sasa anatumikia adhabu baada ya kupokea Pauni za Uingereza milioni 1.35 kutoka kwa Blatter mwaka 2011. Mnamo Juni mwaka huu, Blatter alitangaza kuwa atajiuzulu wadhfa wake kama Rais wa FIFA ingawa yeye pia anatumikia marufuku ya siku 90, Hata hivyo amekanusha kuwa hakushiriki katika kosa lolote la ufisadi katika shirikisho hilo. Platini amekuwa Rais wa UEFA tangu mwaka 2007, alitarajiwa kushinda katika uchaguzi wa kuchukua nafasdi ya Blatter, ambaye sasa ana umri wa miaka 79. Amesema anaamini kuwa ataungwa mkono na washirika mbalimbali katika Soka kushinda kiti cha Urais wa FIFa licha ya kushukiwa ufisadi.