Lugha imeniponza:Mourinho

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, amejitetea kuwa kinachodhaniwa ni lugha mbovu aliyotumia baada ya kushindwa na Southampton ni kwa kuwa Kiingereza si lugha yake ya mama.

Mourinho alifungiwa mechi moja na kupigwa faini ya Pauni za Uingereza 50,000 na shirikisho la Kandanda la Uingereza. Alidai kuwa maafisa wa kandanda nchini humo wanaogopa kuipa timu yake penalti inayostahili. Madai ya Morinho yalitolewa baada ya tume huru maalimu kutoa sababu za adhabu hiyo kutolewa na FA. Kocha huyo machachari wa Chelsea hakuhudhuria kilichomwadhibu lakini alituma taarifa ya maandishi kujitetea. Alikiri kuwa alikosa adabu lakini akakanusha kuwa alitilia shaka hadhi ya refa Robert Madley. Huku akijitetea, Moorinho alisema kuwa makosa yaliyompata ni sawa na yale yaliyowahusu makocha wengine watano wa Premier League. Mbali na kukosoa kiwango cha faini aliyotozwa, Mourinho pia alisema kuwa kupigwa marufuku uwanjani kwa mechi moja, ambako kumeahirishwa kutekelezwa kwa mwaka mmoja, "kulimshangaza". Wenger hakuchukuliwa hatua yo yote alipomsukuma Mourinho katika eneo la wakufunzi katika Stamford Bridge Oktoba mwaka 2014.