Afrika Kusini yatangaza kikosi

Image caption Raman ya Afrika Kusini

Afrika Kusini imetangaza kikosi chake cha kukabiliana na New Zealand bila mabadiliko makubwa katika mechi ya Jumamosi.

Lock Lood de Jager na mshambulizi Bismarck de Pless wamepona majeraha yaliyokuwa yakiwasibu katika robo fainali ambayo walishinda Wales kwa mabao 23 - 19.

Mabadiliko ya kipekee katika kikosi hicho kinamhusu Victor Matfield ambaye ataendelea kukaa kwenye benchi baada ya kupona kifundo.

Matfield, mwenye umri wa miaka 38, atatarajia kushinda katika shindano lake la 126 baada ya kuteuliwa badala ya Pieter-Steph aliyekuwa pia anasubiri kuteuliwa kutoka benchi ya majeruhi.

Naye mchezaji machachari De Jager amepona kiwango cha kuweza kucheza licha ya kupata jeraha mguuni mwisho mwa juma lililopita ingawa Du Plessis atacheza na kidonda alichokipata katika robo fainali kikiwa kimefungwa bendeji.

Itakuwa mara ya kwanza tangu mwaka 2007 kwa Springboks kucheza bila kufanya mabadiliko miongoni mwa wachezaji wake 15 katika mashaindano yake ya Kombe la Dunia.