Arsenal kuvaana na Everton

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Everton
Haki miliki ya picha Getty
Image caption Timu ya Arsenal

Ligi Kuu ya soka ya England itaendelea tena wikendi hii kwa mechi kadhaa, Arsenal watakuwa nyumbani Emirates dhidi ya Everton.

Aston Villa watawakaribisha Swansea City, Leicester itachuana na Crystal Palace, Norwich watakuwa wenyeji wa West Brom, Stoke city watawakaribisha Watford, West Ham watakuwa wenyeji wa Chelsea, mchezo ambao Idhaa ya Kiswahili ya BBC itakutangazia moja kwa moja kupitia ulimwengu wa soka.

Na siku ya Jumapili ligi hiyo itaendelea tena kwa michezo mbalimbali.

Jumamosi 24 Oktoba 2015 Aston Villa v Swansea 15:00 Leicester v Crystal Palace 15:00 Norwich v West Brom 15:00 Stoke v Watford 15:00 West Ham v Chelsea 15:00 Arsenal v Everton 17:30

Jumamosi 25 Oktoba 2015 Sunderland v Newcastle 12:00 Bournemouth v Tottenham 14:05 Man Utd v Man City 14:05 Liverpool v Southampton 16:15

(Muda wa kuanza kwa mechi kwa Saa za Uingereza)