Taifa Stars wanawake kuivaa Zimbabwe

Image caption Taifa Stars ya Tanzania

Timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa magongo kesho jumamosi inatarajia kushuka dimbani kutupa karata yake ya kwanza muda wa saa nane mchana itakapoikabili Zimbabwe katika michuano ya Afrika ya kufuzu fainali za Olompiki zitakazofanyika mjini Rio nchini Brazili mwaka 2016.

Siku ya jumapili Timu ya Wanaume ya Tanzania itaumanana Misri katika mwendelezo wa michuano hiyo.

Na Mashindano hayo yatafikia tamati mapema mwezi Novemba ambapo yanashirikisha Timu mbalimbali kutoka Nigeria,Zimbabwe,Ghana,Tanzania, Namibia, Misri , pamoja na kenya kwa Timu za wanawake na wanaume.