UEFA kuishtaki klabu ya Dynamo Kiev

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Timu ya Chelsea dhidi ya Dynamo Kiev

Shirikisho la Soka barani Ulaya Uefa, limefungua kesi ya kinidhamu dhidi ya klabu ya Dynamo Kiev kutokana na vurugu zilizofanywa na mashabiki wake na mambo ya kibaguzi katika mchezo wa Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea. Katika taarifa yake Uefa imesema itaanza kusikiliza kesi hiyo Octoba 27 mwaka huu. Hiyo sio mara ya kwanza kwa mashabiki wa timu hiyo kuingia matatani kwani katika msimu uliopita Dynamo walitozwa faini ya kufungiwa upande mmoja wa uwanja kwa makosa mawili mojawapo likiwa vurugu na lingine ubaguzi katika mchezo wa michuano ya Europa League.