Urusi yatetea msimamo wake

Haki miliki ya picha epa
Image caption Vladmir Putin

Vladmir Putin ametetea uamuzi wa Urusi wa kuingilia kijeshi nchini Syria akisema hatua hiyo itasaidia kuleta mazingira ya kurejesha suluhisho la kisiasa nchini humo.

Rais Putin amesisitiza kuwa ushindi dhidi ya makundi yanayopigana na wanajeshi wa Rais Assad utasaidia kuanzisha mashauriano ya amani kati ya Serikali na wapinzani aliowataja kama wazalendo.

Alisema Urusi na mataifa ya magharibi yanapaswa kujiona kama washiriki dhidi ya adui wa pamoja - lakini wakati huohuo alilaumu Serikali za Mataifa ya Magharibi kwa kuwa manafiki katika wajibu wao nchini Syria. Alisema mataifa hayo yanawashambulia magaidi wengine lakini wakati huohuo kuwatumia magaidi wengine kwa manufaa yao.