MOJA KWA MOJA: MECHI ZA EPL JUMAMOSI

Bonyeza hapa kupata habari za karibuni zaidi

21:23 Mechi imemalizika. Arsenal wapata ushindi wa 2-1 dhidi ya Everton.

Haki miliki ya picha PA

21:22 Dakika ya 93. Gareth Barry apewa kadi ya pili ya njano.

21: 20 Dakika ya 90. Kieran Gibbs ashindia Arsenal frikiki.

21:19 Kieran Gibbs aingia nafasi ya Alexis Sánchez upande wa Arsenal.

21: 17 Arouna Koné aingia nafasi ya Seamus Coleman upande wa Everton.

21:15 Dakika ya 88, Gareth Barry ananawa mpira.

21:12 Mathieu Flamini atoa kombora lakini linatoka nje upande wa kulia.

21:08 Romelu Lukaku (Everton) atikisa mwamba wa goli la Arsenal kwa mpira wa kichwa. Krosi ilikuwa imetoka kwa Gareth Barry. Dakika ni ya 80.

21:04 Dakika ya 76. Gareth Barry ajaribu kupitisha eneo la hatari, lakini Kevin Mirallas ameotea.

21:03 Kona yapigwa. Mpira wa kichwa wa Brendan Galloway waenda nje.

21:01 Alex Oxlade-Chamberlain atupa mpira nje. Ni kona ya Everton.

20:58 Everton wamuingiza Kevin Mirallas nafasi ya Aaron Lennon. Ni dakika ya 70 sasa.

20:55 Olivier Giroud wa Arsenal apewa kadi ya njano ya kucheza vibaya.

20:34 Ramiro Funes Mori aingia nafasi ya Phil Jagielka aliyeumia. Mambo bado ni Arsenal 2-1 Everton.

20:30 Mechi yasitishwa kwa muda baada ya Phil Jagielka wa Everton kuumia.

Kipindi cha pili chaanza.

Ni muda wa mapumziko sasa

20:17 BAOOO!Arsenal 2-1 Everton

Ross Barkley (Everton) atoa kombora la kushoto ambalo limeenda na kutua kona ya kushoto ndani ya goli. Amesaidiwa na Gerard Deulofeu.

Haki miliki ya picha AFP

20:07 BAOOOO! Arsenal 2-0 Everton

Laurent Koscielny (Arsenal) afunga bao kwa kichwa dakika ya 39 baada ya kufikia krosi ya Santiago Cazorla.

20:06 Seamus Coleman wa Everton afanya madhambi. Alexis Sanchez kupiga frikiki.

20:05 BAOOOO!

Arsenal 1-0 Everton

Olivier Giroud afunga kwa kichwa dakika ya 36 baada ya kufikia krosi ya Mesut Özil.

19:30 Sasa ni Arsenal nyumbani Emirates dhidi ya Everton

18:54 Mechi zilizomalizika

West Ham 2- 1 Chelsea

Aston Villa 1- 2 Swansea

Norwich 0-1 West Brom

Stoke 0-2 Watford

Leicester 1-0 Cyrstal Palace

18:52 Jon Obi Mikel aonyeshwa kadi ya njano kwa kumfyeka Dimitri Payet.

18:44 West Ham 2-1 Chelsea

Chelsea wafanya badiliko lao la mwisho. Baba Rahman aingia nafasi ya Cesar Azpilicueta.

18:42 BAOOOO!

Aston Villa 1-2 Swansea City

Andre Ayew afungia Swansea dakika ya 87.

Haki miliki ya picha Reuters

18:39 West Ham 2-1 Chelsea

Radamel Falcao aingia nafasi ya Ramires. Mechi imesalia dakika nane hivi.

18:36 BAAOOOOO!

West Ham 2-1 Chelsea

Andy Carroll, aliyeingia kama nguvu mpya, aifungia West Ham.

Haki miliki ya picha AFP

18:34 West Ham 1-1 Chelsea

Chelsea wajiweka hatarini baada ya Asmir Begovic kutouchukua vyema mpira wa kurudishwa nyuma wa John Terry. Kipa alazimika kuutupa nje na kuwa kona. Terry aondoa kona hiyo eneo la hatari.

18:32 West Ham 1-1 Chelsea

Cheikhou Kouyate amchezea visivyo Ramires kutoka nyuma na kuonyeshwa kadi ya njano.

18:27 West Ham 1-1 Chelsea

West Ham wamtoa shujaa wao aliyewafungia bao Mauro Zarate na kumuingiza Andy Carroll.

18:26 Stoke 0-2 Watford

Almen Abdi aongezea Watford la pili.

Haki miliki ya picha Getty Images

18:23 Aston Villa 1-1 Swansea

Gylfi Sigurdsson asawazishia Swansea kupitia frikiki.

18:18 BAOOOO!

Aston Villa 1-0 Swansea

Jordan Ayew, afungia Villa bao lake la kwanza.

18:15 BAOOOOO!

Leicester 1-0 Crystal Palace

Bao lafungwa na Jamie Vardy

Vardy amejiunga na Thierry Henry, Alan Shearer, Ian Wright, Mark Stein, Emmanuel Adebayor, Ruud van Nistelrooy na Daniel Sturridge katika kufunga mabao mfululizo mechi za Ligi ya Premia. Wote walifunga mabao mechi saba mfululizo.

Van Nistelrooy ndiye mwenye rekodi kwa kufungia Man Utd bao kila mechi kwa mechi 10 mwaka 2003.

18:13 BAOOOOOO!

West Ham 1-1 Chelsea

Bao limefungwa na Gary Cahill. Amelifunga kwa kichwa baada ya kuchapwa kwa kona.

18:02 Mourinho afukuzwa uwanjani. Fabregas ameondolewa nafasi yake pakaingia Obi Mikel.

Mourinho amefukuzwa baada yake kuomba aruhusiwe kuingia chumba cha refa Jon Moss wakati wa mapumziko. Sasa anakaa na chumba cha wakurugenzi uwanjani.

Haki miliki ya picha Reuters

18:01 BAOOOO!

Norwich 0-1 West Brom

Bao limefungwa na Salomon Rondon

18:00 Timu zote zimerejea uwanjani

17:45 Ni muda wa mapumziko sasa

Matokeo kufikia sasa

West Ham 1-0 Chelsea

Stoke 0-1 Watford

17:44 Mkasa kwa Chelsea

Nemanja Matic afukuzwa uwanjani kwa kumfanyia madhambi Diafra Sakho. Fabregas na Costa nao waonyeshwa kadi za manjano kwa kulalamika.

Haki miliki ya picha Other

17:43 BAOOOO! Stoke 0-1 Watford

Bao la Troy Deeney

17:42 Cesc Fabregas atumbukiza mpira wavuni, lakini bao lakataliwa kwa kuwa alikuwa ameotea.

17: 39 BAOOOO!

Kkatika ligi ya daraja la pili, Shola Ameobi afunga bao mechi yake ya kwanza kuchezea Bolton Wanderers.

17:36 West Ham 1-0 Chelsea

Kurt Zouma akaribia sana kufunga bao kwa kichwa. Adrian na Carl Jenkinson wauzuia mpira kuvuka mstari wa goli.

17:36 Nemanja Matic aonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea visivyo Diafra Sakho.

17:17 BAOOOOOO!

West Ham 1-0 Chelsea

Mauro Zarate

West Ham watwaa uongozi kupitia kona. Mpira wa kichwa wa Ramires umeenda moja kwa moja kwa Mauro Zarate.

17:14 Aston Villa 0-0 Swansea

Federico Fernandez apoteza nafasi ya mwaka upande wa Swansea baada ya kona iliyopigwa na Jonjo Shelvey.

17:11 Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa anapoteza nafasi nzuri.

17:00 West Ham 0-0 Chelsea

Chelsea wanaanzisha mchezo. Uwanja umerowa kutokana na mvua ambayo imekuwa ikinyesha.

16:59 Kikosi cha Chelsea: Uwanjani: Begovic, Zouma, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic, Willian, Fabregas, Hazard, Costa

Benchi: Amelia, Baba Rahman, Mikel, Loftus-Cheek, Oscar, Traore, Falcao

16:58 Kikosi cha West Ham: Uwanjani: Adrian, Jenkinson, Tomkins, Collins, Cresswell, Noble, Kouyate, Zarate, Payet, Lanzini, Sakho

Benchi: Randolph, Carroll, Valencia, Obiang, Ogbonna, Jelavic, Antonio

16.57 Klabu ya Chelsea leo imo ugenini West Ham ikijaribu kufufua kampeni yake Ligi ya Premia msimu huu baada ya kuandikisha matokeo yasiyo ya kuridhisha tangu mwanzo wa msimu.

Mechi zote za leo:

Aston Villa v Swansea 15:00

Leicester v Crystal Palace 15:00

Norwich v West Brom 15:00

Stoke v Watford 15:00

West Ham v Chelsea 15:00

Arsenal v Everton 17:30

Haki miliki ya picha epa