New Zealand yatinga fainali

Image caption Timu ya taifa ya Rugby ya New Zealand

Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya New Zealand wamefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya dunia

Mabingwa hao watetezi wamefika hatua hiyo baada ya kuishinda timu ya Afrika kusini kwa pointi 20 kwa 18.

Mpaka mapumziko Afrika kusini walikua wanaongoza kabla kurudi kipindi cha pili na kufanya vyena na kuibuka kidedea.

New Zealand wanamsubiri mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya pili utakaozikutanisha Australia na Argentina.