Australia yatinga fainali za Raga dunia

Image caption Australia yaichapa Argentina mchezo wa Raga

Timu ya taifa ya Australia ya mchezo wa raga imetinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia la mchezo huu.

Australia walishuka dimbani kukabiliana na timu ya taifa ya Argentina na kuibuka kidedea kwa pointi 29 dhidi ya 15 za wapinzania wao.

Mchezaji mahiri wa Australia Adam Ashley-Cooper, aliisaidia timu yake kupata alama 13 za kuongoza mchezo huu wa nusu fainali.

Australia itapamba na New Zealand katika mchezo wa fainali utakaofanyika Octoba 31 huku michezo ya mshindi wa tatu ikifanyika Octoba 30.