Gianni Infantino kuwania urais Fifa

Image caption Katibu mkuu wa shirikisho la soka ulaya,uefa, Gianni Infantino

Katibu mkuu wa shirikisho la soka barani ulaya (Uefa) muitaliano Gianni Infantino amejitosa kwenye kinyanganyiro cha kuwania kiti cha uraisi wa shirikisho la soka dunia Fifa.

Infantino, anaunga na boss wa Uefa aliyesimamishwa Mfaransa Michel Platini, kuwania nafasi hiyo kuongoza chombo hicho cha soka.

Huku rais wa shirikisho la soka la Asia Sheikh Salman bin Ebrahim Al Khalifa pia amethibitisha kuwania cheo hicho.

Wengine wanaowania kiti hicho cha urais wa Fifa ni Mosima Gabriel maarufu kama Tokyo Sexwale, wa Afrika Kusini Prince Ali Bin al-Hussein wa Jordan, David Nakhid, wa Trinidad and Tobago, Jerome Champagne Musa Bility na Segun Odegbami wa Nigeria