WTA :Muguruza, Kerber washinda

Haki miliki ya picha epa
Image caption Nyota wa Tenis Garbine Muguruza

Nyota wa Tenesi Garbine Muguruza wa Hispania na Angelique Kerber wa ujerumani wameanza vyema michuano ya wanawake ya tenesi inayofanyika huko Singapore.

Garbine Muguruza anayeshika nafasi ya tatu kwa ubora wa mchezo huo alimchapa mpinzani wake Lucie Safarova kwa seti 6-3 7-6 7-4.

Nae Angelique Kerber akamshinda nyota namba tano kwa ubora Petra Kvitova kwa jumla ya seti 6-2, 7-6 7-3.

Michuano hii imegawanyika katika makundi mawili , huku Nyota namba moja kwa ubora duniani Serena Williams anakosekana kwenye michuano hii kutokana na kuwa majeruhi.