Blatter: Tulijadili Kombe la Dunia la Urusi 2018

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Blatter amekiri kuwa katika kikao cha kamati ya FIFA mwaka wa 2010 urusi ilijadiliwa kama mwenyeji wa kombe la dunia la 2018

Rais wa FIFA Sepp Blatter amekiri kuwa uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 wa Urusi ulijadiliwa hata kabla ya kura ya kutangazwa kwa wenyeji wa kombe la dunia.

Rais huyo ambaye kwa sasa amepigwa marufuku na kamati ya uadilifu ya FIFA ameiambia shirika la habari la Urussi TASS, kuwa jopo zima la kutoa uwenyeji wa fainali za kombe la dunia ulikaa na kujadili mwaka wa 2010 nia ya kuzishirikisha mataifa hasimu Urusi na Marekani katika maandalizi ya kombe la dunia.

''hata hivyo shinikizo kutoka kwa wadau ndio iliyobadilisha matokeo ya uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2022 kutoka Marekani na kwenda Qatar'' Alisema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 79.

Image caption Rais huyo raia wa Uswissi anatumika marufuku ya siku 90 kwa pamoja na msaidizi wake ambaye ni rais wa shirikisho la soka la bara Ulaya Michel Platini

Rais huyo raia wa Uswissi anatumika marufuku ya siku 90 kwa pamoja na msaidizi wake ambaye ni rais wa shirikisho la soka la bara Ulaya Michel Platini.

Wawili hao wamekanusha madai yote dhidi yao.

Na alipoulizwa kama ilikuwa ni kosa kutoa uwenyeji wa kombe la dunia wa mwaka wa 2018 na 2022 kwa pamoja Blatter alisema

''Nia yetu ilikuwa kuandaa makala yajayo ya fainali za kombe la dunia katika mataifa mawaili yenye uwezo mkubwa duniani.''

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption ''Nia yetu ilikuwa kuandaa makala yajayo ya fainali za kombe la dunia katika mataifa mawaili yenye uwezo mkubwa duniani.'' Blatter

''Wanakamati walishauri kuwa ni bora fainali zijazo zichezwe Urusi kwa sababu fainali hizo hazijawahi kuandaliwa Mashariki mwa bara Uropa.''

''2022 tungerejea Marekani., ila kwa sababu moja au nyingine ushawishi ulisababisha kura 4 muhimu za wanakamati kutoka bara ulaya kuendea Qatar.''

Tayari utoaji zabuni za uwenyeji wa fainali hizo mbili zinachunguzwa na utawala wa Uswisi.