Van Gaal amtaka Martial kushambulia

Haki miliki ya picha PA
Image caption Louis Van Gaal

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Louis Van Gaal anahisi kuwa mchezaji Anthony Martial ataongoza safu ya mashambulizi katika siku za usoni.

Mchezaji huyo wa miaka 19, aliyesajiliwa kutoka klabu ya Monaco kwa pauni milioni 36, mnamo mwezi Agosti amefunga mabao matano msimu huu, lakini amekuwa akichezeshwa upande wa kushoto, ikiwemo mechi ya jumanne dhidi ya CSKA Mosco.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Anthony Martial

"ni kijana mdogo sana, lakini ni bora iwapo ataimarika kama mshambuliaji", alisema Van Gaal.