RIPOTI ZA MOJA KWA MOJA:MAN UTD vs WEST BROM

RIPOTI ZA MOJA KWA MOJA ZA LIGI NCHINI UINGEREZA

7.56pm:Matokeo ya mechi nyengine

Bournemouth 0 - 1 Newcastle FT

Leicester 2 - 1 Watford FT

Man Utd 2 - 0 West Brom FT

Norwich 1 - 0 Swansea FT

Sunderland 0 - 1 Southampton FT

West Ham 1 - 1 Everton FT

Stoke v Chelsea 17:30

7.53pm:Na mechi inakamilika hapa huku manchester United ikiibuka kidedea.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Gooal

7.49pm:Gooooooooooooal katika dakika moja ya ziada Juan Mata aifungia manchester united bao la pili.

7.45pm:Anthony Martial aangushwa katika eneo la miguu kumi na mbili na refa akaonyesha mkwaju wa penalti na kutoa kadi nyekundi kwa beki McColney.Mata anapiga penalti

Image caption Michael Carrick

7.44pm:Matokeo kufikia sasa

Bournemouth 0 - 1 Newcastle FT Leicester 2 - 0 Watford L Man Utd 1 - 0 West Brom L Norwich 1 - 0 Swansea L Sunderland 0 - 1 Southampton L West Ham 1 - 1 Everton L Stoke v Chelsea 17:30

View Live Scores

7.42pm:Luois Van Gaal afanya mabadiliko..nadhani ya kujaribu kulitetea bao lile

7.41pm:Manchester United inacheza gusa ni guse lakini mabao hayaongezeki do.

7.26pm:Dakika ya 70 Manchester United 1 West Bromwich )

Image caption Kocha Pulis akiwaambia wachezaji wake kusonga mbele ili kupata bao la kusawazisha.

7.21pm:West Brom wich licha ya kufungwa hawajaanza kujitokeza hapa ili kulishambulia lango la Man United na badala yake wanasalia wakilinda lango lao.

7.20pm:Kufikia sasa Matokeo ya EPL

Leicester 1 - 0 Watford L

Man Utd 1 - 0 West Brom L

Norwich 0 - 0 Swansea L

Sunderland 0 - 0 Southampton L

West Ham 1 - 1 Everton L

7.11pm:Goooooal dakika ya saba katika kipindi cha pili.Lingard anamwangalia kipa yuko wapi halafu anauweka pembeni mpira na kuiweka kifua mbele Manchester United

Kipindi cha pili cha Mechi

Image caption Ashley Young

6.48pm:Na kipindi cha kwanza cha mpira kinakamilika

6.46pm:Chris Smalling amchezea vibaya mchezaji wa West Brom.Chris Brunt anapiga mpira wa adhabu ule kuelekea Man United.Kona

6.44pm: Martial gooooal la Manchester United wafanya mashambulizi hapa lakini Mc Colney aokoa mpira

6.42pm:Timu zote mbi zinaonyesha jitihada hapa lakini hakuna ilioshambulia lango la mwengine.

Licha ya gusa ni guse ile ya Manchester United hawajalishambulia lango la West Brom

Image caption Anthony Martial

6.40pm:Matokeo kufikia sasa

Bournemouth 0 - 1 Newcastle FT

Leicester 0 - 0 Watford L

Man Utd 0 - 0 West Brom L

Norwich 0 - 0 Swansea L

Sunderland 0 - 0 Southampton L

West Ham 1 - 0 Everton L

Image caption Louis Van Gaal

6.36pm:Dakika ya 36 kipindi cha kwanza hakuna timu ilioona lango la mwenzie

6.36pm:Kona kuelekea Manchester United na hatari inaondolewa katika lango la manchester United

6.32pm:Wachezaji wa West Brom wanaonekana wakifukuza kivuli na hata wakipata mpira ule wanaupoteza kwa urahisi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption West Brom

6.30pm:Rooney anapiga kona kuelekea West Bromwich lakini Swweinsteger anapiga juu na mpira unatoka nje na kuwa goal kick

6.28pm;Anakwenda Martial hapa lakini beki huyo wa West Brom anazuia na kuanza kuwasomea wenzake.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Martial

6.27pm:Martial anaushika mpira hapa

6.26pm:Mipira inafika katika boksi la West Brom Wich lakini hakuna wachezaji ambao wanaweza kuutia wavuni.

Image caption West Bromwich

6.24pm:Mpira unarushwa kuelekea lango la man United.unapigwa kwa David Degea ambaye hajapata kazi nzito kufikia sasa

6.22pm:Dakika ya 22 Manchester united 0 West Brom Wich 0

6.21pm:Fauli inapigwa kuelekea West Brom Wich dakika ya 21

6.20pm:Kufikia sasa hakuna shambulizi lolote lililofanywa na West Brom huku Wachezaji wa Man United wakiendelea kutafuta bao la kwanza

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Yuan Mata na Wayne Rooney

6.17pm:Yuan Mataaaaaa lo nje akosa mkwaju ambao umetoka sentimita chache nje ya goaal.lo.. ingekuwa mengine

6.14pm:Mpira unatoka anayekwenda kurusha ni Marcus Rojo.Rojo anamrushia Chris Smalling anauchukua lakini Darren Fletcher anamsukumua Yuan Matta

6.12pm:Manchester United wanacheza kwa kasi hapa wakicheza gusa ni guse na kusonga mbele

6.11pma:Wachezaji wote wa West Brom Wich wamerudi nyuma hapa

6.10pm:Manchester United inaanza kwa kufanya mashambulizi katika timu ya West Brom.

Image caption Man United vs West Brom

6.00pm:Mechi inaanza

5.58pm:Kocha wa West Brom Tony Pulis: Itakuwa mechi ngumu kabisa ukizingatia fedha zilizotumiwa na Luois kununua wachezaji

5.57pm:Kocha wa Manchester United Louis van Gaal: Ningependa kuwaelezea mashabiki kunizomea mimi na sio wachezaji"

5.56pm:Kikosi cha West Bromwich

13 Myhill 25 Dawson 23 McAuley 06 Evans 11 Brunt 07 Morrison 05 Yacob 24 Fletcher 14 McClean 29 Sessegnon 33 Rondón

Substitutes

03 Olsson 04 Chester 08 Gardner 17 Lambert 18 Berahino 19 McManaman 21 Lindegaard

Ref: Mike Dean

5.55pm:Kikosi cha Manchester United

01 de Gea 18 Young 12 Smalling 17 Blind 05 Rojo 16 Carrick 31 Schweinsteiger 08 Mata 10 Rooney 35 Lingard 09 Martial

Substitutes

04 Jones 07 Depay 20 Romero 21 Herrera 28 Schneiderlin 43 Borthwick-Jackson 44 Pereira

Manchester United vs West Brom Wich Albion

Haki miliki ya picha Associated Press
Image caption Newcastle

5.38pm:Na Mechi inakamilika hapa ikiwa Newcastle imeibuka mshindi kwa bao moja dhidi ya Bournemouth

5.28pm:Bournemouth waendelea kumiliki mpira lakini wameshindwa kabisa kuvunja ngome ya Newcastle

5.16pm:Aotea pale Papis Demba Cisse baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Moussa Sissoko.

5.02pm:Kocha wa Newcastle Steve McClaren aonekana pale akiwa ameridhika na bao lile moja

5.01pm:Bournemouth inatawala mchezo ikiwa na asilimia kubwa ya umiliki wa mpira lakini safu ya ulinzi ya Newcastle inakataa kufunguka ili kusawazisha.

4.45pm:Timu zote zinajaribu kuona lango la mwengine lakini bado safu zao za ulinzi zakataa

Kipindi cha pili Bournemouth 0 Newcastle 1

04:30pm Mchezaji Harry wa Bournemouth ampatia pasi safi Joshua King lakini refa aonyesha kibendera akisema ameotea.

04:23pm:Mkwaju wa Joshua King (Bournemouth) waokolewa .

04:20pm: Joshua King (Bournemouth) asababisha mkwaju wa adhabu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Newcastle vs Bournemouth

04:19pm: Fabricio Coloccini (Newcastle United) apata mkwaju wa adhabu katika wingi ya kushoto.

04:16pm: Junior Stanislas (Bournemouth).Acheza vibaya hapa na kusababisha mkwaju wa adhabu

04:15pm: Vurnon Anita (Newcastle United) apata mkwaju wa adhabu katika wingi ya kulia..

04.11pm:Goooooooal Goal! Bournemouth 0, Newcastle United 1. MKwaju wa mguu wa kushoto wa Ayoze Pérez (Newcastle United) kutoka katikati ya boxi wamuwacha kipa wa Bournemouth bila jibu

Jaribio jingine la mkwaju wa Andrew Surman [Bournemouth)

03:48pm Harry Arter (Bournemouth) apata mkwaju wa adhaby katika wingi ya kushoto.

3.45pm:Mechi kati ya Newcastle na Bournemouth

12.00:Ligi ya Uingereza

Image caption Ligi ya Uingereza

Ligi kuu ya England itaendelea kutimua vumbi leo kwa nyasi za viwanja saba kuwaka moto.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Chelsea wenye mwendo wa kusuasua watakua ugenini katika dimba la Britannia kuwakabili Stoke City.

Manchester United watakua katika uwanja wao wa Old Trafford kuwalika West Bromwich Albioni.

Wagonga nyundo wa london West Ham watawaalika The Toffees Everton, huku paka weusi wa Sunderland wakiwakaribisha watakatifu wa Southampton katika uwanja wa Light.

Michezo mingine ni

Bournemouth na Newcastle

Leicester na Watford

Norwich na Swansea