Manchester United yaisakama West Brom

Image caption Man United dhidi ya West Brom

Jesse Lingard alifunga bao lake la kwanza akiichezea Manchester United huku timu hiyo ya Louis Van Gaal ikiishinda West Bromwich.

Winga Lingard mwenye umri wa miaka 22 alifunga bao zuri alipomwangalia kipa wa West Brom na kuuficha mpira ule katika wavu na kuiweka kifua mbele timu hiyo.

Mchezaji wa ziada wa West Brom Saido Berahino alikosa fursa nzuri kusawazisha baada ya kupiga kichwa nje akiwa karibu na goli.

Juan Mata alifanya mambo kuwa salama kwa upande wa Manchester United baada ya kufunga mkwaju wa penalti baada ya Anthony Martial kuangushwa na Gareth McAuley ambaye alipewa kadi nyekundu.

Ushindi huo unaiweka Manchester United katika nafasi ya nne katika jedwali la ligi ya Uingereza huku West Bromwich ikiwa katika nafasi ya 12.