Ronaldo anaishi maisha ya 'upweke'

Haki miliki ya picha
Image caption Cristiano Ronaldo anaishi kwa 'upweke'

Mtayarishi wa sinema inayoangazia maisha ya mwanakandanda wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo anasema kuwa nyota huyo anaishi maisha ya upweke mno.

James Gay-Rees ambaye alipata umaarufu kwa kuandaa filamu kuhusu ya maisha ya mwendesha magari ya langalanga Senna, raia wa Brazil, anasema kuwa Cristiano hana marafiki wengi.

"Ana marafiki wachache mno''

Haki miliki ya picha AP
Image caption '' Kule kujituma kunamtaka awe na nidhamu ya hali ya juu mwenyewe.'' anasema James

''Mara nyingi Cristiano huwa na familia na jamaa yake'' alisema James.

''Nafikiri kuwa kule kujituma kunamtaka awe na nidhamu ya hali ya juu mwenyewe. Hivyo analazimika kujinyima vitu vingi kiasi ambacho hakiaminiki katika macho ya mtu wa kawaida''.

Filamu hiyo imewalazimu James na kundi lake la wapiga picha wamekuwa wakirekodi kila kitu katika maisha ya Ronaldo kwa kipindi cha mwaka mmoja hivi.

Kilichomshangaza James ni unyenyekevu wa nyota huyo mshindi mara tatu wa tuzo la mchezaji bora duniani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Licha ya kuwa na unajiri mkubwa Ronaldo " ana marafiki wachache mno'' anasema produsa wake

''Kwa hakika kuwa nyota wa hadhi kama yake inataka kuwa mnyenyekevu wa kupindukia,'' alisema James.

James alikanusha dhana ya kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid na Ureno ni mjeuri sio kweli.

''Huyu bwana ni mnyenyekevu mno na machache wa maneno.''

Haki miliki ya picha epa
Image caption 'mara nyingi anashinda na familia na jamaa wake' James

''Amini usiamini alitizama filamu hii mara kadhaa wala hakuwa na ila, alifurahia sana filamu yenyewe licha ya kuwa ilikuwa na vipengee fulani ya kumkashifu.''

Kwa hakika iliaweze kuendelea kucheza kwenye kiwango hicho cha kimataifa Cristiano analazimika kufanya kazi ya ziada kufanya mazoezi kuepuka anasa na kuepuka mambo yanayoweza kumuondolea umakini wa mchezo alisema James.

James alikuwa mmoja wa maprodusa waliotengeneza filamu kuhusu maisha ya mwanamuziki marehemu Amy Winehouse iliyojulikana kwa jina Amy.