Waliopanga mechi Nepal washtakiwa kwa uhaini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nahodha Sagar Thapa na kipa Ritesh Thapa,Wanatuhumiwa kwa kupanga matokeo ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia 2011

Wachezaji 5 wa timu ya taifa ya Nepal wamefikishwa mahakamani katika mji mkuu wa Kathmandu kujibu mashtaka ya uhaini.

Watano hao wakijumuisha nahodha wa timu hiyo na mlinda lango wameshtakiwa kwa kosa la kupanga matokeo ya mechi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waliopanga mechi Nepal washtakiwa kwa uhaini

Nahodha Sagar Thapa na kipa Ritesh Thapa,Wanatuhumiwa kwa kupanga matokeo ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia 2011 ambapo Nepal ilishindwa.

Watano hao walikamatwa mwezi uliopita.

Haki miliki ya picha bharat bandhu thapa
Image caption Wachunguzi walitahamaki walipogundua kiwango kikubwa mno cha fedha katika akaunti za wachezaji hao.

Wachezaji hao wamekanusha madai dhidi yao huku wakidai wanasingiziwa tu.

Bhadrakali Pokharel, msajili mkuu wa mahakama maalum ya Kathmandu aliliambia shirikisho la habari la AFP kuwa wanakabiliwa na shtaka la kusaliti nchi na hivyo watashatkiwa kwa uhaini.

Pokharel anasema kuwa kwa mujibu wa sheria ya 1989 ''mtu yeyote anayesaliti nchi na kuhujumu uhuru wa Nepal atahukumiwa kifungo cha maisha jela.''

Haki miliki ya picha AFF
Image caption Watano hao walikamatwa mwezi uliopita.

Wachunguzi walitahamaki walipogundua kiwango kikubwa mno cha fedha katika akaunti za wachezaji hao.

Uchunguzi wa msingi ulibaini kuwa pesa hizo zilikuwa zimetoka kwa wacheza kamari maarufu wanaodaiwa kupanga mechi Mashariki mwa bara Asia.

Kiongozi wa mashtaka ya umma anatawaka wahukumiwe kunyongwa.