Fainali za Olimpiki kuchezewa Maracana

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Olimpic Brazili

Shirikisho la FIFA limeutangaza uwanja wa Maracana kuwa ndio utakaotumika katika fainali za michezo ijayo ya Olimpiki zitakazofanyika Brazil.

Mchezo wa ufunguzi wa makundi kwa wanawake utafanyika Agosti 3 katika Uwanja wa Olimpiki katika mji wa Rio de Janeiro.

Mchezo wa ufunguzi wa wanaume nao utafanyika Agosti 4 katika uwanja wa Brasilia, ambao ndio uwanja ghali zaidi kujengwa na ulitengenezwa kwa ajili ya Kombe la Dunia la lililofanyika nchi humo mwaka 2014.

Viwanja saba vitatumika katika michezo hiyo vikiwemo viwili katika mji wa Rio de Jeneiro, pamoja na Arenas ulioko Belo Horizonte, Brasilia, Manaus, Salvador na Sao Paulo.