Michezo ya mchujo kombe la dunia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kikombe, kombe la Dunia 2018

Michezo ya raundi ya pili ya kuwania tiketi ya kucheza kombe la dunia la mwaka 2018 litakalofanyika urusi kuendelea leo.

Timu ya taifa ya Kenya Harambe Stars watakuwa wenyeji wa visiwa vya Cape Verde huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa funyika siku ya Jumanne ijayo.

Libya watakua wenyeji wa Rwanda, wakati Angola watakua nyumbani kuwakaribisha Afrika ya kusini.

Michezo mingine itayopigwa leo hii ni Niger na Cameroon Liberia na Ivory Coast Swaziland na Nigeria Mauritania na Tunisia Madagascar na Senegal Comoros na Ghana