Timu tano zasonga hatua ya makundi

Image caption Kikosi cha Uganda kimesonga mbele

Timu za Uganda, DR Congo, Morocco, Guinea na Gabon zimesonga mbele katika hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya Kombe la Dunia.

Uganda, wakicheza nyumbani katika uwanja wa Mandela waliifunga Togo 3-0 na hivyo wakawa wameshinda kwa jumla ya mabao 4-0 ambapo mchezo wa kwanza walishinda kwa bao 1-0.

Gabon nao wakasonga mbele katika hatua ya makundi kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Msumbiji.

Nao Zambia, wakawachapa Sudan kwa 2-0 na kufuzu kwa makundi kwa jumla ya mabao 3-0 huku mabao ya jana yakifungwa na Lubambo Musonda na Winston Kalengo.

DR Congo walitoka sare ya 2-2 na Burundi huko kwao lakini wamesonga mbele baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-2 huko Bujumbura.

Morocco nao wamefuzu licha ya kufungwa 1-0 jana na Equatorial Guinea baada ya wao kushinda mechi ya kwanza 2-0.

Timu hizi 6 zilizofuzu zitaungana na nchi nyingine 14 zitakazofuzu Jumanne na kupangiwa makundi matano ya timu 4 kila kundi.

Mshindi mmoja wa kila kundi atafuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi.