Ireland yaifunga Bosnia-Herzegovina

Image caption Ireland yatinga fainali michuano ya Ulaya

Timu ya taifa ya Jamuhuri ya Ireland,imetinga katika fainali za michuano ya Ulaya baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Bosnia-Herzegovina.

Winga Jonathan Walters ndiye aliyekua shujaa kwa kufunga mabao yote mawili bao la kwanza akilifunga katika dakika ya 24 kwa mkwaju wa penati,kisha Walters akashindilia msumari wa pili katika dakika ya 70.

Jamuhuri ya Ireland imesubiri kwa miaka sita kuweza kupata nafasi hiyo ambapo mwaka 2009 walikosa nafasi hiyo dakika za mwisho baada ya kufungwa na ufaransa bao la utata lilofungwa kwa mkono na mshambuliaji Thierry Henry'

Katika mchezo wa kwanza timu hizi zilikwenda sare ya kufungana bao 1-1 hivyo Ireland imepita kwa jumla ya mabao 3-1.

Leo kutachezwa michezo miwili ya mwisho itakayotoa timu mbili za mwisho zitakazoshiriki michuano ya Euro hapo mwakani nchini Ufaransa.

Slovenia itakua mwenyeji wa Ukraine katika mchezo wa kwanza Ukraine iliishinda Slovenia kwa mabao 2-0.

Denmark itakipiga na Sweden huku mchezo wa kwanza Sweden iliitambia Denmark kwa kuwafunga mabao 2-1.