Hofu ya ugaidi yafuta mchezo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Polisi nchini Ujerumani wakiwa katika hali ya ulinzi baada ya mechi kuvunjwa

Mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Ujerumani na uholanzi uliokua ufanyike usiku wa kuamkia jumatano umefutwa kwa hofu ya mashambulio ya ugaidi.

Mchezo huu ulikua ufanyike katika uwanja wa Hdi Arena,Hannover, haukuweza kufanyika baada ya kuwa na taarifa kulikua na mpango wa kufanyika mashambulizi ya ugaidi wakati wa mchezo huo.

Mkuu wa polisi wa jiji la Volker Kluwe aliiambia BBC "Kulikua na mpango wa kufanyika ulipuaji katika uwanja huo".

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alikua ahudhurie mchezo huo katika uwanja wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 49,000.

Mchezo mwingine uliofutwa leo hii kwa hofu ugaidi ni kati ya Ubelgiji na Hispania uliokua ufanyike nchini Ubelgiji.