LeRoy ajiuzulu kuifunza Congo Brazaville

Haki miliki ya picha getty
Image caption Aliyekuwa Kocha wa Congo Brazaville, Claude LeRoy

Kocha mfaransa Claude LeRoy, aliyekua mkufunzi wa kikosi cha timu ya taifa ya Congo Brazzaville,amejiuzulu kuifundisha timu hiyo.

LeRoy mwenye umri wa miaka 67 aliuambia uongozi wa soka wa kocha wa Congo uamuzi huo muda mfupi baada ya kuiongoza timu hiyo kuingia hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kombe la dunia kwa kuifunga Ethiopia kwa mabao 2-1

Kumekua na tetesi huenda kocha huyu akarudi kuifundisha timu ya taifa ya Cameroon, ambayo imemtimua kocha wake Volker Finke.

LeRoy,ana historia ya kuwa Kocha aliyeshiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa mara nane na akitwaa taji hilo mwaka 1988, akiwa na kikosi cha Cameroon.