Rufaa ya Blatter, Platini yagonga mwamba

Haki miliki ya picha RIA Novosti
Image caption Aliyekuwa Rais wa Uefa Michel Platini

Rufaa iliyokatwa na Rais wa Fifa aliyesimamishwa Sepp Blatter pamoja na raisi wa Uefa Michel Platini kupinga kusimamishwa kwa siku tisini zimekataliwa na kamati ya rufaa ya shirikisho hilo la soka.

Blatter na Platini, walisimamishwa mwezi octoba na kamati ya maadili ya Fifa kwa muda wa siku tisini kupisha uchunguzi juu ya tuhuma za rushwa zinazowakabili viongozi hao wa juu.

Wote wamekana makosa yao na sasa watakata rufaa katika mahakama ya usuluhishi wa michezo (CAS)

Platini anatarijia kuwasilisha utetezi wake katika mahakama ya michezo ya Cas siku ya ijumaa kwa mujibu wa mwanasheria wake Thibaud d'Ales.