Sweden, Ukraine zafuzu Euro 2016

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bostjan Cesar akipatia goli Slovenia

Timu za taifa za Sweden na Ukraine zimekua timu za mwisho kuzufu kwa michuano ya ulaya mwaka 2016 nchini Ufaransa.

Sweden wakicheza ugenini walikwenda sare ya mabao 2-2 dhidi ya Denmark, huku wakifanikiwa kufuzu baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa 2-0.

Mshambulia Zlatan Ibrahimovic ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya Sweden huku yale ya Denmark, yakifungwa na Yussuf Poulsen na Jannik Vestergaard.

Ukraine nao wakatinga kwenye fainali za Ulaya licha ya kwenda sare ya bao 1-1 na Slovenia, katika mchezo wa kwanza Ukraine walishinda kwa mabao 2-1.

Timu 24 zilizofuzu kushiriki michuano hiyo ya ulaya ni wenyeji Ufaransa,

Albania, Austria, Belgium, Croatia, Czech Republic, England, France, Germany, Hungary, Iceland, Italy, Northern Ireland, Poland, Portugal, Republic of Ireland, Romania, Russia, Slovakia, Spain, Sweden, Switzerland, Turkey, Ukraine, Wales.