Eddie Jones kocha mpya Raga,England

Eddie Jones leo anakuwa kocha mpya timu ya Raga ya Uingereza na kuwa na raia wa kwanza wa kigeni kuifundisha timu hiyo.

Raia huyo wa Australian mwenye umri wa miaka 55,amekwisha kamilisha kuwasilisha vielelzo mhimu vya ajira yake hiyo mpya na kiongozi mkuu wa chama Ian Ritchie

Kocha huyo wa zamani wa Australia ameamua kuachana na klabu ya Afrika Kusini ambayo amekuwa na mkataba nayo wa muda mrefu hadi sasa.

Jones anachukua nafasi ya Stuart Lancaster aliyeachia nafasi yake kuinoa klabu hiyo ya Raga ya Uingereza baada ya kushindwa katika michuano ya kombe la Dunia ya Raga 2015.