La Liga: Kivumbi cha El Clasico Jumamosi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mchezo wa jumamosi utakutanisha mahasimu wakubwa Real Madrid na Barcelona

Ligi kuu ya Uhispania nayo itaendelea siku ya jumamosi baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa huku mchezo mkubwa ukiwa ni wa mahasimu Real Madrid na Barcelona.

Mchezo huu wa wapinzani hawa uliobatizwa jina la El Clasico utachezwa katika dimba la Santiago Bernabeu huku mashabiki wapatao 80,000 wakitazama mchezo huo katika uwanja huo.

Huku kukiwa na ahadi ya ulinzi wa kutosha kutoka kwa Polisi na wanausalama, hii inakuaja baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi nchini Ufaransa wiki hii.

Mvuto mkubwa wa mchezo huu ni kuwepo kwa nyota Cristiano Ronaldo wa real Madrid huku Leonel Messi wa Barca akiwa na hatihati baada baada ya kutoka kwenye majeruhi ya goti.

Mbali na mchezo wa El Clasico kutapigwa michezo mingine ya ligi hii:

  • Real Sociedad na Sevilla
  • Espanyol na Malaga
  • Valencia na Las Palmas