Mchezaji apewa marufuku ya miaka 4

Image caption Mchezaji Ademi Arjani wa Dinamo Zagreb kushoto

Kiungo wa kati wa klabu ya Dinamo Zagreb Arijan Ademi amepigwa marufuku ya miaka minne kwa kupatikana na dawa za kusisimu misuli wakati wa ushindi wa timu yake dhidi ya Arsenal katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Raia huyo wa Macedonia mwenye umri wa miaka 24 alicheza dakika 90 wakati wa ushindi huo wa kushangaza dhidi ya Arsenal huko Zagreb mwezi Septemba.

Ademi alisema:Sina hatia na sijafanya makosa yoyote.Sijui nisemeje kufuatia marufuku hiyo.Najihisi vibaya kwa sasa.

Kocha Zoran Mamic alisema kuwa klabu hiyo itakata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa ''kufedhehesha''

Mamic aliuambia mtandao wa Zagreb:Ademi na wataalam walidhihirisha kwamba dawa anazotumia ziliathiriwa na kitu fulani na hakujua dawa aliyokuwa akitumia.

''Hiyo ndio sababu siwezi kuelewa hatua hii iliochukuliwa na Uefa.Marufuku ya miaka minne ni upuzi.''

''Je, Uefa ingeviadhibu vipi vilabu kama vile Arsenal, Bayern,Manchester United ama vilabu vyengine vikubwa? Tutampigania na kesi yake kwa sababu Ademi ni kijana mwenye kipaji na naibu nahodha wa timu.