MOJA KWA MOJA:Watford dhidi ya Man United

Ripoti za moja kwa moja za mechi za ligi ya Uingereza jumamosi

5.37pm:Na Mechi inakamilika hapa ikiwa Manchester United imepanda hadi katika kilele cha ligi baada ya kuinyuka Watford mabao 2-1 ugenini.

5.35pm:Dakika zimeongezwa nne hapa na Watford wanajaribu kusawazisha lakini hali si hali

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bastian Shweinsteiger

5.30pm:Gooooooal Bastian Schweinsteiger aiweka kifua mbele manchester United hapa ikiwa imesalia dakika moja.manchester United 2 Watford 1

Image caption Deeney Trey

5.28pm:Gooooal nahodha Deeney Troy anasawazisha hapa na kufanya mambo kuwa watford 1 manchester United 1

5.26pm:Zikiwa zimesalia dakika tano ili mechi kukamilika watford inajipatia penalti

Image caption Memphis Depay

5.23pm:Mambo yalivyo kwa sasa manchester United ipo kileleni mwa ligi ya Uingereza huku Manchester City na Arsenal wakitarajiwa kucheza baadaye.

5.18pm:Juan Mata atoka na mahala pake kuchukuliwa na Lingaard

5.16pm:la la la Watford wailemea Hanchester United hapa na ni kipa De gea pekee anayewaokoa hapa.Mpira unaendelea kwa kasi.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Golkipa David De Gea aibeba Manchester United katika kipindi cha pili

5.03pm:Wachezaji wa Watford sasa waonekana kufufuka baada ya kulemewa katika kipindi cha kwanza.Na sasa mjinga akierevuka mwerevu yu mashakani.hakukosea aliytunga msemo huo kwani Man United sasa wako mashakani.

4.59pm: Man United waepuka bao hapa baada ya kuvamiwa na Watford huku timu hii ya nyumbani ikitafuta bao kwa udi na uvumba.

Image caption David De Gea

4.57pm:Goooal la la De gea aokoa kwa mara pili hapa na sasa watford wamiliki mpira na kuisukuma nyuma man United

Image caption nahodha wa kilabu ya watford Deeney Trey

4.56pm:United wanaendelea kuwasukuma wachezaji wa watford

4.45pm:Na kipindi cha pili kinaanza kwa kasi hapa Watford wakitafuta bao la kusawazisha huku nayo Manchester ikitafuta bao la

Na kipindi cha kwanza cha mechi chakamilika

4.30pm:Watford yapata kona yao ya kwanza,lakini mabeki wa Man United wasimama imara na kuondoa hatari.

4.28pm:Kipa wa watford afanya masihara hapa na karibia Juan Mata apate bao la bwerere lakini kipa anaurudia mpira na kuupiga nje.

Image caption Hivi ndivyo hali ilivyo

4.26pm:Dakika ya 41 Watford 0 man United 1

4.18pm:Mchezaji wa watford amchezea vibaya Andres Herrea hapa na refa anaonekana akimuonya.

Image caption Ashely Young

4.17pm:Manchester Unbited yapata kona.lololo... karibia ajifunge mwenyewe huyu mchezaji wa Watford lakini beki anaondoa hatari hiyo.

Image caption Juan Mata wa Manchester United akikabwa na mchezaji wa watford

4.06pm:Watford wakosa bao la wazi hapa baada ya kusalia na mabeki wawili pekee wa United.

4.03pm:Dakika ya 18 Watford 0 Manchester United 1 bao lilofungwa na kijana wa miaka 21 Mephis Depay

Image caption Chris Smalling

4.00pm:Vijana wa Watford wanaamka hapa baada ya kufungwa na wanajaribu kuipenya ngome ya United lakini mabeki wa United wanaoongozwa na Smalling wanakataa.

3.58pm:Kabla ya bao lake Mkufunzi wa manchester united louis Van Gaal alikuwa amesema kwamba anatarajia mengi kutoka kwa mampehis Depay ambaye alikuwa amifungia klabu hiyo bao moja tangu ajiunge na timu hiyo.

Image caption Memphis Depay akisheherekea baada ya kufunga bao

3.56pm:Gooooooal .Memphis Depay aiweka Manchester United kifua mbele hapa kunako dakika ya 10 baada ya kupata krosi safi kutoka kwa Ander Herrera.Manchester United 1 Watford 0

3.52pm:Kumbuka Manchester United inacheza bila vioungo wake imara wayne Rooney na Anthony martial ambao wamejerihiwa

Image caption Washambuliaji wa watford wana matumaini ya kuicharaza United

3.45pm:Mechi inaanza kati ya watford na manchester United hapa ambapo timu ya watford imevalia jezi za rangi ya manjano huku wageni wao manchester United wakivalia jezi nyekundu.

3.00pm:Kikosi cha Watford.

Image caption Kikosi cha watford

Watford XI: Gomes; Nyom, Cathcart, Britos, Anya; Capoue, Watson; Abdi, Jurado, Deeney; Ighalo.

Image caption Watford dhidi ya man United

2.45pm:Kikosi cha Manchester United

Image caption Kikosi cha man United

Man Utd XI: De Gea; Young, Jones, Smalling, Blind; Schneiderlin, Schweinsteiger; Mata, Herrera, Lingard; Memphis.