Gareth Bale:Tuko tayari kuibwaga Barca

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Gareth Bale katikati

Mchezaji wa Real Madrid Gareth Bale amesema kuwa yuko tayari kukabiliana na Barcelona wakati ambapo klabu yake inajiandaa kupimana nguvu na wapinzani wao Barcelona katika mchuano wa Jumamosi wa El Classico.

Raia huyo wa Wales mwenye umri wa miaka 26,alipata jeraha la nyonga mnamo mwezi Oktoba na alikosa kucheza mechi nne kabla ya kurudi tarehe 8 Novemba ambapo klabu yake ilishindwa na Sevilla.

''Nimekuwa nje nikiuguza jeraha kwa wiki sita,kwa hivyo sijapata fursa ya kucheza mechi nyingi msimu huu'',alisema.lakini sasa najihisi niko tayari kwa mechi hii''.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gareth Bale na Christiano Ronaldo

Bale alikosa kucheza katika mechi ya kirafiki kati ya Wales na Uholanzi ambapo timu hiyo ilishindwa 3-2.

Real Madrid inacheza mechi hiyo ikiwa nyuma ya viongozi Barcelona kwa pointi tatu.