Leicester waongoza jedwali la EPL

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Vijana wa Jurgen Klopp, walitawala Etihad na kuondoka na ushindi wa 4-1.

Baada ya kugawana muda wa kuwa kileleni mwa ligi kuu ya soka nchini uingereza, hatimaye Vigogo Arsenal na Manchester city wamesalimu amri.

Hii ni baada ya West Brom kuishangaza Arsenal kwa kuilaza 2-1 ugani Hawthorns.

Vijana wa Jurgen Klopp, walitawala Etihad na kuondoka na ushindi wa 4-1.

Hata baada ya kutangulia kutikisa wavu,kupitia Oliver Giroud, goli la Rondon na bao la kujifunga la Mikel Arteta ziliipa West Brom alama tatu muhimu na kuiteremsha Arsenal hadi nafasi ya nne.

Santi Carzola alipiga nje mkwaju wa penalti baada ya Sanchez a kuchezewa 'ngware' na kupoteza nafasi ya kipekee ya Arsenal kusawazisha mambo n kugawanya alama.

Uwanjani Etihad, vijana wa Jurgen Klopp

walionyesha kufufuka baada ya kuonyesha ujasiri dhidi ya matajiri wa Manchester City , The Citizens.

Wanasamba, Firminho na Coutinho walishirkiana kuwatesa mabeki wa City na kumpa Klopp ushindi wa pili dhidi ya klabu kubwa zaidi baada ya kuilaza Chelsea 3-1 wiki chache zilizopita.

Bao la Kun Aguero halikutosha kuizuia Liverpool kusafiri bila alama tatu.

Leicester city na Machester United ndio wanaongoza ligi hiyo kwa alam 28 na 27 mtawalia.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wenger hajui aseme nini ?

Masaibu ya Aston villa yanaendelea huku klabu hiyo ikiwa mkiani na alama 5.

Jedwali la ligi kuu ya Uingereza
1. Leicester 13 8 28
2. Man United 13 10 27
3. Man City 13 14 26
4. Arsenal 13 12 26
5. Tottenham 12 10 21
6. West ham 12 7 21
7. Everton 13 8 20
8. Southampton 13 5 20
9. Liverpool 13 2 20
10. Crystal Palace 12 2 19