Van Gaal kumrudisha Ronaldo Old Trafford

Image caption Van Gaal kumrudisha Ronaldo Old Trafford

Kocha wa Manchester United imethibitishwa anajaribu kumrejesha mshambuliaji matata wa Real Madrid Cristiano Ronaldo Old Trafford .

Louis van Gaal amethibitisha kuwa wanawafuatilia wachezaji kadhaa akiwemo Ronaldo kwa nia ya kuwarejesha Old Trafford ilikuiimarisha ushindani wake msimu huu.

''Kwa hakika tunawafuatilia wachezaji kadhaa sio tu Ronaldo.''

''Kwa kiwango kikubwa wengi wa wachezaji tunaowataka hawaachiki''

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Van Gaal anamtaka Ronaldo kurejea Old Trafford

''Kumhusu Ronaldo, kwa hakika tunasubiri thibitisho kwa udi na uvumba'' alisema Van Gaal.

Mshambulizi huyo machachari aliihama man United katika msimu wa 2009 akielekea Real Madrid kwa kitita cha pauni milioni 80.

Mreno huyo ameibuka kuwa mfungaji hodari wa mabao wa klabu hiyo bingwa mara kumi barani ulaya.

Ronaldo ambaye ametawazwa kuwa mchezaji bingwa wa dunia mara tatu aliweka rekodi ya kuifunga Real Madrid mabao 323.

Rekodi ya awali ilikuwa inashikiliwa na Raul.

Haki miliki ya picha AFP Getty Images
Image caption Ronaldo ameifunga Real Madrid mabao 323.

Alipotua Santiago Bernabéu Ronaldo alishinda taji moja la La Liga ,taji moja la ubingwa wa bara Ulaya mbali na vikombe kadha vya mashindano ya Uhispania katika kipindi cha miaka 6.

Ronaldo aliwasili Old Trafford akitokea Sporting Lisbonkwa kitita cha pauni milioni £12.24 pekee.

Akiwa Old Trafford Ronaldo alifunga mabao 118 katika mechi 292.