Wanariadha waandamana Kenya

Image caption Wanariadha waandamana Kenya

Kundi la wanariadha waliojawa na hamaki limevamia makao makuu ya shirikisho la riadha nchini Kenya AK na kufunga milango wakilalamikia ubadhirifu na ufisadi katika jumba la Riadha mjini Nairobi.

Wanariadha hao waliwazuia maafisa wa shirikisho hilo la AK kuingia afisini mwao.

Walikuwa wamebeba mabango ya kukashifu uongozi duni na ufisadi uliokithiri afisini humo.

Maandamano hayo yanafuatia madai ya hivi punde zaidi kuwa takriban dola laki saba za Marekani $750,000, fedha za ustawishaji wa riadha nchini Kenya ziliporwa na maafisa wakuu watatu wa shirikisho hilo.

Fedha hizo zilikuwa zimetolewa na kampuni ya kutengeneza bidhaa za michezo Nike.

Nike ndio iliyopewa zabuni ya kutengeza sare za timu ya taifa ya riadha.

Haki miliki ya picha b
Image caption Wanariadha kadha wakenya wamepatikana na hatia ya matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini

Naibu mwenyekiti wa shirikisho hilo David Okeyo tayari anachunguzwa na idara ya kupambana na ufisadi.

Okeyo amekana madai hayo dhidi yake.

Vilevile wanariadha hao wanailaumu shirikisho hilo la Atheltics Kenya kwa kupokea hongo kutoka kwa mawakala wanaoshukiwa kuwashawishi wanariadha nchini humo kutumia madawa ya kutitimua misuli yaliyopigwa marufuku duniani.

Kenya ni moja ya mataifa yaliyotajwa kuwa na tatizo sugu la utumiaji wa dawa hizo za kuongeza nguvu mwilini na shirikisho la kupamabana na matumizi ya dawa hizo duniani WADA.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kenya ni moja ya mataifa makubwa zaidi duniani katika riadha

Afisa aliyeongoza uchunguzi wa shirikisho la riadha duniani Dick Pound alishauri WADA iangazie kurunzi yake kwenye afisi za shirikisho la riadha la Kenya baada ya kuitimua Urusi.

Wanariadha hao wanadai kuwa maafisa wa AK wamekuwa wabinafsi sana na sasa wanatishia posho lao.

Kundi hilo la wanariadha linawataka waondoke afisini na pahala pao kuchukuliwa na wanariadha wa zamani