Novak Djokovic ambwaga Roger Federer

Haki miliki ya picha no credit
Image caption Novak Djokovic

Mchezaji tenisi namba moja Duniani kutoka Serbia, Novak Djokovic amemaliza msimu wake kwa ushindi dhidi ya Roger Federer.

Ushindi huo umemfanya kuweka rekodi ya taji la nne mfululizo la mashindano ya ATP.

Djokovic alifanikiwa kushinda kwa seti 6-3, 6-4 katika dakika 80 za mchezo huko London, na aliweza kusahihisha makosa yake baada ya mechi ya mwanzo ya makundi kufungwa na Roger Federer.

Mpaka sasa Djokovic anamaliza mwaka huu kwa kushinda mataji 11 yakiwemo ya matatu ya Gland slam, na kwa upande wake Roger Federer amesema hakuna furaha yoyote katika upande ulioshindwa ila ni vizuri kushiriki kuliko kutoshiriki kama mwaka uliopita.